Mara ya mwisho Christian Ericksen kuonekana katika michezo ya kimataifa ilikuwa ni miezi mingi iliyopita ilikuwa katika michuano ya EURO 2020 mchezo ambao Ericksen alidondoka uwanjani baada ya kupata shambulio moyo liliyomfanya kukaa nje kwa muda mrefu.
Jana kwa mara ya kwanza amerudi kuipigania timu yake ya taifa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi uholanzi na kufanikiwa kufunga goli moja kwenye kipigo cha 4-2 kutoka kwa uholanzi goli lililomfanya kufikisha magoli 37 katika michezo ya kimataifa.
Alikataliwa kucheza katika ligi kuu ya pale italy Seria A kutokana na uwepo wa sheria ambazo hazimruhusu mchezaji mwenye kifaa cha ICD kucheza ligi hio amepata dili la miezi 6 kuichezea klabu ya Brentford ya pale EPL.