Aliyewahi kuwa msaidizi binafsi wa muigizaji Will Smith, Brother Bilaal amefanya mahojiano na blogger Tasha K, ambapo alisimulia kisa cha Will Smith kumpiga mke wake baada ya kumfumania akifanya mapenzi na mwanamuziki Marc Anthony.
“Mambo yalitokea siku nyingi kiasi, Will aliingia nyumbani kwake na kumkuta mke wake akifanya mapenzi na Marc Anthony kwenye kochi, alichokifanya ni kumshushia kipigo kilichomfanya alazwe hospitali ya nyumbani ili kuzuia taarifa zisiwafikie watu wa nje’’, alisema Brother Bilaal.
Will Smith alijua kuwa mkewe na Marc Anthoy wana mahusiano ya mapenzi, lakini kitendo cha kuwakuta wakifanya mapenzi nyumbani kwake ilikuwa ni dharau iliyomfanya Will kushindwa kuzuia hasira yake.
Taarifa hiyo ambayo imeanza kusambaa muda mfupi baada ya mahojiano hayo kufanyika wiki iliyopita, imekanushwa na Will & Jada Smith.
Hii sio mara ya kwanza kwa Brother Bilaal kuja na taarifa zinazohusu mambo binafsi ya Bosi wake wa zamani. Wiki iliyopita alionekana kwenye video akisimulia jinsi alivyomkuta Will Smith akifanya mapenzi ya jinsia moja na Duane Martin.