RONALDO AREMA CHECHE MAN.UNITED


🎙️Nilitaka kwenda Man City lakini Sir Alex Ferguson alinipigia na kuniambia sipaswi kwenda City nami sikutaka kumkatalia, nikaufuata moyo wangu na nikarejea Old Trafford. 

🎙️Nilidhani nitaona vitu tofauti ndani ya United lakini nimeshangaa mambo mengi ni yale yale tangu nilipokuwa nina miaka 20,21,22 teknolojia imebadilika ila United tupo pale pale. 

🎙️Nahisi kusalitiwa na Man United, kuna baadhi ya watu hawataki niwepo hapa na sio msimu huu tu ni tangu msimu uliopita wanataka niondoke, mimi naiheshimu sana klabu hii na Mashabiki wake. 

🎙️Sina heshima yoyote kwa Erik Ten Haag kwakuwa yeye haniheshimu, kama wanataka kufanya mabadiliko ikiwemo kuniondosha ni sawa ila wanapaswa kubadili vitu vingi sana ndani ya United. 



🎙️Sijui kwanini Wayne Rooney ananikosoa sana, pengine kwakuwa bado nacheza muda mrefu tena kwenye ushindani mkubwa kuliko yeye, hilo sifahamu. 

Post a Comment

Previous Post Next Post