KONDOMU ZA BURE KENYA HAZIPATIKANI TENA



Mashirika ya kiraia nchini Kenya yanalalamikia uhaba wa muda mrefu wa kondomu za bure kote nchini.

Bidhaa hizo zinazookoa maisha kwa kawaida huagizwa na kusambazwa bila malipo lakini kutokana na ushuru mkubwa wa kuagiza - wasambazaji hawapati tena Kenya kondomu za bure.

Kwa miaka miwili iliyopita, mipira hiyo- kwa kawaida kwenye pakiti ya kijivu au nyekundu, imekuwa vigumu kupatikana katika vituo vya afya vya umma kote nchini.

"Kwa nini tunapaswa kutoza ushuru bidhaa zinazotolewa bila malipo?

Kupitia njia hii kutaleta maafa katika nchi ambayo haiwezi kufadhili mfumo wetu wa afya.

Tunapaswa kuamua kama tunataka kondomu au kodi kwa sababu mara tu wafadhili watakapojiondoa, basi tunaangamia." Dk. Samuel Kinyanjui, mkurugenzi wa AIDS Healthcare Foundation (AHF) nchini humo aliwaambia waandishi wa habari.

Taifa hilo la Afrika Mashariki linarekodi takriban maambukizi mapya 34,000 ya VVU kila mwaka.

Lakini, tangu 2020, kumekuwa na ongezeko thabiti.

Kondomu zimekuwa muhimu katika kampeni za kuzuia VVU na magonjwa mengine ya zinaa kama vile Kisonono na Klamidia.

Pakiti moja ambayo ina kondomu tatu huuzwa kwa dola moja ya Marekani - bei ambayo ni ya juu mno kwa baadhi ya watu.

Post a Comment

Previous Post Next Post