JAMBAZI SUGU AKAMATWA DAR



Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limemkamata Jambazi sugu anayeitwa  Johson Omary Mchome dereva bodaboda ambaye muda mwingine anajulikana kwa jina la Rashid Amirakon ambaye mwaka huu amekuwa na akituhumiwa yeye na wenzake kwa vitendo vya kihalifu na kinyanganyi kwa kutumia silaha Maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Tarehe 24/11/2022 jioni wananchi walifanikisha kupatikana kwa taarifa juu ya kuwepo kwa watu ambao wamekuwa wakifanya matukio katika Jiji la Dar Es Salaam,wakati wa ufuatiliaji mtuhumiwa alikatwa maeneo ya Kisarawe akijiandaa kukutana na wenzake muda mfupi baada ya kugundua amezunhira Polisi alitoa bastola yake iliyokuwa katika begi dogo jekundu na kuanza kuwashambulia polisi ndipo polisi walijibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi kwenye mguu na kumkamata.

Post a Comment

Previous Post Next Post