WAZIRI UMMY ATAMANI JINA LA MIREMBE KUBADILISHWA



Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amesema anatamani jina la Hospitali ya Afya ya Akili ya Mirembe iliyopo Dodoma kubadilishwa jina kutokana na imani za watu wanavyofikiria wakisikia mtu anapelekwa katika Hospitali hiyo.

Waziri Ummy amesema "Natamani sana jina la Mirembe libadilishwe kwa kweli kwa sababu ukienda pale Mirembe unaonekana we ni chizi wewe una matatizo,Afya ya akili ni tatizo linalo mpata kila mtu tunataka mtu wa afya ya akili akienda kupata matibabu anaenda kupatiwa sehemu yenye staha kwa sababu afya ya akili ni kama magonjwa mengine ya mwili.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Oktoba 28,2022 Jiji Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Post a Comment

Previous Post Next Post