MHE.MABULA AAHIDIWA USHIRIKIANO



Wakili Peter Begga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Leo tarehe 12.10.2022 ametembelea Ofisi ya Mbunge Jimbo la Nyamagana kwa lengo la kujitambulisha baada ya kushinda uchaguzi Septemba Mosi. 2022. Wakili Begga ambaye amepokelewa na Katibu wa Mbunge Bi. Florah Magabe, na kupata fursa ya ku sign kitabu cha wageni, ametumia adhra hiyo kumpongeza Mhe Stanslaus Mabula kwa kazi kubwa anayoifanya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi 2020-2025 Jimboni na kuahidi ushirikiano wa dhati kipindi chote Cha uongozi wake huku akionesha shahuku ya kuifanya Nyamagana kuwa ya Kijani kwa kuimarisha chama sanjari na kuisimamia serikali.

Naye Bi. Florah Magabe amesema Mhe. Mabula yupo Nje ya Mkoa wa Mwanza kikazi, hivyo amemshukuru kutembelea Ofisi hiyo ya wananchi huku akimpongeza kuamininwa na Chama Cha Mapinduzi kushika Hatamu ndani ya Miaka mitano, na kuahidi ofisi ya Mbunge kumpatia ushirikiano wa dhati iwe jua iwe mvua. *”Tumemaliza Uchaguzi na wewe Wewe ndio Mwenyekiti tutakuunga mkono kwa 100% kwa mstakabali wa ustawi wa Chama Cha Mapinduzi kuzidi kushika Dora.”* Alisema Bi. Magabe.

Wakili Begga Katika ziara hiyo aliambatana na ujumbe wa viongozi waandamizi Wilaya ya NYamagana akiwemo Katibu wa CCM Wilaya Geofrey R Kavenga, Mwenezi Wilaya Comrade Mustapha BANIGWA, Mwenyekiti UWT Wilaya Mhe. Witnesses K Makale, Mwenyekiti Umoja wa Vijana Mussa Magana, Katibu UWT Getrude D Mboyi, katibu Wazazi Wilaya Bi. Mariam Msangi ambao wote kwa pamoja walipata FURSA ya ku sign kitabu.

Post a Comment

Previous Post Next Post