APIGWA SHOTI BAADA YA KUKATA NGUZO YA UMEME KWA KUTUMIA SHOKA



Juma Kigodi mwenye umri wa miaka 22 Mkazi wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora amejeruhiwa vibaya maeneo tifauti ya mwili wake baada  ya kupigwa na shoti ilitoka kwenye nguzo ya umeme ambayo aliikata kwa kutumia shoka.

Akielezea kinaga ubaga namna tukio hilo lilivyo tokea Myendaji wa Kata wa Nkiniziwa Hamis Bandu amesema Kigodi alitenda tukio hilo usiku wa kuamkia Oktoba 10,2022.



Kabla ya kukata nguzo huo Kijana huyo alirusha waya juu ya nyaya za umeme ili azivute nyaya zilizo kuwa zimeshikiliwa na nguzo sababu ya kufanya hivyo ni kuukata umeme ili apate uraisi wa kuikata nguzo hiyo bila zoezi hilo lili shindikana kwani umeme ulikuwa hauja kata na wakati anaanza kuikata nguzo ndipo nyaya zikamuangukia na kupigwa na shoti.

Baada ya kutokea tukio hilo Kigodi alikimbikwa katika Hosptali ya karibu ili kupatiwa matibabu.

Post a Comment

Previous Post Next Post