RAPA BABY CINO AUWAWA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA JELA

Mauaji bado yanaendelea kuwamaliza marapa wadogo katika kiwanda cha mziki wa Hip Hop na Rap huko Marekani baada ya Rapa mdogo Baby Cino kupigwa risasi na kufariki muda mfupi baada ya kutoka jela siku ya jumatano baada ya kukamatwa akiwa na silaha.

Akiwa kwenye gari dogo aina ya Nissani alilokuwa akiendesha na washikaji zake katika maeneo ya Palmeto ExpressWay walishambuliwa na watu walio kuwa kwenye gari nyeusi iliyokuwa kwenye mwendokasi na kushababisha kifo cha Baby Cino na majeraha kwa rafiki zake.
Taarifa za awali zinaeleza mauaji hayo yametekelezwa na kundi la wahuni linajulikana kama Miami Streets Gangs ambalo pia wiki chache zilizo pita lilifanya mauaji ya jamaa mmoja anayejulikana kama Wavy Navy Pooh huko Miami.

Post a Comment

Previous Post Next Post