EVERTON WAKATWA POINTI 10 EPL

 


.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Everton imepunguziwa pointi 10 baada ya kubainika kuwa wamekiuka kanuni za faida na uendelevu za Ligi ya Primia.

Adhabu hiyo ndiyo kubwa zaidi ya kimichezo katika historia ya mashindano hayo na kuwaacha Everton wakiwa nafasi ya 19 kwenye jedwali kwa jumla ya pointi nne.

Klabu hiyo ilisema "ilishtushwa na kukatishwa tamaa" na uamuzi wa "kutokuwa na usawa na usio wa haki".

Everton wamesema wanakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Ligi ya Primia ilipeleka Everton kwa tume huru mnamo mwezi Machi lakini haikufichua maelezo mahususi ya madai ya ukiukaji wa klabu hiyo.

Everton ilichapisha hasara za kifedha kwa mwaka wa tano mfululizo mnamo mwezi Machi baada ya kuripoti nakisi ya pauni milioni 44.7 mwaka 2021-22.

Vilabu vya Premier League vinaruhusiwa kupoteza £105m kwa kipindi cha miaka mitatu na Everton ilikiri kukiuka kanuni za faida na uendelevu kwa kipindi kinachoishia 2021-22.

Kufuatia kusikilizwa kwa kesi yao kwa siku tano mwezi Oktoba, tume ilipata kuunga mkono Ligi ya Premier kwamba hasara za Everton katika kipindi hicho zilifikia £124.5m.

Katika taarifa yake, Everton ilisema: "Klabu haitambui matokeo ya kushindwa kuchukua hatua kwa nia njema na haielewi sababu hii kuwa madai yaliyotolewa na Ligi Kuu wakati wa kesi hiyo.

"Ukali na ukubwa wa vikwazo vilivyowekwa na tume sio haki na si mwafaka wa ushahidi uliowasilishwa.

"Klabu pia itafuatilia kwa hamu kubwa maamuzi yaliyotolewa katika kesi nyingine zozote zinazohusu kanuni za faida na uendelevu za Ligi Kuu."

Kupunguzwa kwa pointi kunatokea wakati wa kutokuwa na uhakika mkubwa kwa Everton.

Mnamo mwezi Septemba, mmiliki Farhad Moshiri alikubali kuuza hisa zake 94% katika klabu kwa mfuko wa wawekezaji wa Marekani 777 Partners.

Mchakato huo unapitia taratibu za udhibiti na kabla ya uamuzi huu, vyanzo vilisema ulikuwa uko tayari kukamilika mwezi ujao.

,

'Kutowajibika - Hali ambayo Everton imejitakia yenyewe

Ikieleza ni kwa nini Everton imepunguziwa pointi nyingi, tume hiyo ilisema katika sababu zake zilizoandikwa ni matumizi makubwa - hasa kwa wachezaji wapya - pamoja na kutokuwa na uwezo wa kuuza wachezaji, na kumaliza ligi ikiwa na matokeo mabaya kuliko ilivyotarajiwa.

Kumaliza kwa klabu hiyo katika nafasi ya 16 mnamo 2021-22 kulisababisha hasara ya mapato yaliyotarajiwa ya takriban £21m, sababu zinaeleza.

Tume iliongeza: "Hamu ya kueleweka ya Everton kuboresha uchezaji wake uwanjani (kujaza nafasi ya kiungo wa kati asiyekuwepo, kama Bw Moshiri alivyoweka ushahidi) ilichochea kujiweka hali hiyo kwenye suala la kanuni za faida na uendelevu.

"Hilo lilisababisha kupita kiwango cha £105m kwa £19.5m.

" Hali ambayo Everton imejipata imejitakia yenyewe. Kiwango cha juu zaidi ni muhimu. Matokeo yake ni kwamba hatia ambayo Everton imepatikana nayo ni kubwa.

"Tunazingatia ukweli kwamba mwenendo wa kanuni za faida na uendelevu wa Everton katika kipindi cha miaka minne ni chanya, lakini hatuwezi kupuuza ukweli kwamba kushindwa kufuata kanuni hiyo kulitokana na Everton kutowajibika ikifanya maamuzi huku ikiamini kuwa mambo yatakwenda sawa."

Mwenyekiti wa tume hiyo, David Phillips KC, pia alirejelea maombi ya fidia ya kifedha kutoka kwa klabu za sasa za Ligi Kuu ya Uingereza Burnley na Nottingham Forest na timu zilizoshuka daraja msimu uliopita, Leicester City, Leeds United na Southampton.

Phillips alisema "ameridhika kwamba vilabu vilivyotuma maombi vina madai ya kulipwa" - lakini akabainisha kuwa tume hiyo haina "mamlaka ya kisheria" badala yake ni "jukumu la Ligi Kuu kuleta na kushtaki malalamiko".

Adhabu kubwa zaidi katika historia ya Primia League - lakini je Everton inaweza kuendelea?

Katika historia ya Ligi Kuu ni vilabu vingine viwili pekee vilivyowahi kupunguziwa pointi.

Middlesbrough ilipunguziwa pointi tatu kwa kushindwa kushiriki mechi dhidi ya Blackburn msimu wa 1996-97, huku mwaka 2010 Portsmouth ilipokonywa pointi tisa baada ya kuingia kwenye uongozi.

Hakuna klabu iliyoweza kuepuka kushuka daraja kufuatia adhabu hizo.

Makato hayo yanaifanya Toffees kuwa sawa na Burnley iliyo mkiani kwa pointi nne baada ya mechi 12.

Kikosi cha Sean Dyche, ambacho kilimaliza msimu uliopita kwa pointi mbili juu ya nafasi za kushuka daraja, kilikuwa kinashika nafasi ya 14 katika jedwali - na pointi nane mbele ya timu tatu za chini.

Mara tatu za awali ambapo klabu ya Primia League imekuwa na pointi chache kama nne baada ya mechi 12, Everton mwaka 1994-95 ndiyo pekee iliyojipata katika hali hiyo.

Manchester City ndiyo klabu nyingine pekee iliyoshtakiwa na Ligi Kuu ya Uingereza kwa ufujaji wa fedha, ilipopelekwa kwenye tume huru kwa madai ya ukiukaji wa sheria zaidi ya 100 kati ya 2009 na 2018.

Washindi mata tatu City walishtakiwa Februari – kabla ya Everton - na kesi hiyo bado inaendelea.

Wakati huo huo, Chelsea inaweza kuchunguzwa zaidi na mamlaka ya soka kuhusu ripoti za malipo yanayohusiana na mmiliki wa zamani wa klabu hiyo Roman Abramovich.

Chelsea ilitozwa faini ya pauni milioni 8.6 na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa mwezi Julai kwa "kuwasilisha taarifa za kifedha ambazo hazijakamilika" kati ya 2012 na 2019 kama sehemu ya suluhu ya kukiuka Sheria za fedha za Fifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post