WAFUNGA OFISI YA KIJIJI,KISA KUDHARAULIWA NA VIONGOZI

Wananchi wa kijiji cha Nkumba kata ya Kwankonje wilayani Handeni mkoani Tanga, wamefunga ofisi ya Serikali ya eneo hilo wakishinikiza viongozi wao kujiuzuru kutokana na kutowashirikisha kwenye shughuli za maendeleo.

Wakizungumza kwenye mkutano maalum wa kijiji cha Nkumba ulioitishwa na diwani kwa lengo la kuwasikiliza jana Alhamisi ya April 6, 2023 wananchi hao wamedai kuwa kuna uvunaji wa mbao na shughuli nyingine za maendeleo zinafanyika kijijini hapo ila mapato yake hayajulikani yanakwenda wapi.

Mmoja wa wananchi hao Aweso Dyambala amesema yapo matatizo yaliosababisha wao kufunga ofisi ambapo la kwanza ni kutoshirikishwa kuhusu mapato na mchakato wa kuwepo muwekezaji wa kuchimba madini bila kushirikisha wananchi wa eneo hilo.

“Sisi wananchi na Serikali tulikubaliana kuuza eneo la msitu ili fedha itakayopatikana ijenge zahanati, msitu umenunuliwa kwa Sh800, 000 hazijulikani zilipo na hakuna maelezo ya kutosha” amedai.
Mwenyekiti kijiji cha Nkumba, Shabani Athumani amekiri ni kweli wamevuna mbao ila na ilipitishwa na halmashauri ya kijiji na lipo kihalali, ila ameshangazwa na kundi hilo linalokataa wasifanye kazi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kwankonje, Ramia Nkandulo amesema anafahamu uvunwaji wa mbao kwaajili ya shule na Serikali ya kijiji, ila kuhusu kufungwa ofisi hajui tatizo limeanzia wapi.

Post a Comment

Previous Post Next Post