ARTETA,TRIPPIER,CASEMIRO KWENYE TETESI ZA USAJILI LEO


TH

CHANZO CHA PICHA

Newcastle United wamekataa ofa ya Bayern Munich kumnunua beki Kieran Trippier, 33. (Sky Sports)

Trippier ana nia ya kujiunga na Bayern Januari hii ikiwa wanaweza kukubaliana na Magpies. (Times - usajili unahitajika)

Newcastle pia wamekataa ofa ya mkopo kwa mshambuliaji wa Uingereza Callum Wilson kutoka Atletico Madrid lakini wanaweza kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ikiwa ofa ya kudumu itatolewa (Mail)

Kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho yuko kwenye mazungumzo na klabu ya Saudia ya Al-Shabab kuhusu kuchukua nafasi ya meneja wao baada ya kutimuliwa na Roma. (Sportitalia - kwa Kiitaliano)

TH

CHANZO CHA PICHA,

Mustakabali wa kiungo wa kati wa Brazil Casemiro katika klabu ya Manchester United baada ya msimu huu uko mashakani kwani klabu hiyo inaamini ni bora kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31.(Star)

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ana hamu ya kumleta mshambuliaji wa Ajax na Uholanzi Brian Brobbey mwenye umri wa miaka 21 Old Trafford wakati wa dirisha la uhamisho la Januari. (Sky Sports Ujerumani)

Beki wa Uhispania Aymeric Laporte aliondoka Manchester City na kujiunga na Al-Nassr msimu uliopita wa joto na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anasema kuna wachezaji wengi ambao hawajaridhika kucheza kwenye Ligi ya Saudia. (AS - kwa Kihispania)

TH

CHANZO CHA PICHA,

Matthijs de Ligt yuko tayari kuondoka Bayern Munich msimu huu wa joto huku Manchester United wakifufua tena nia yao ya kumnunua mlinzi huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24.(Mirror)

Mshambulizi wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 20, ana kipengele cha kumuachilia cha pauni milioni 43 katika mkataba wake ambacho kitaanza kutumika msimu huu wa joto. (Sky Sports Ujerumani)

Everton wataazimia kumshikilia kiungo wa kati wa Mali Abdoulaye Doucoure, 31, ambaye anahusishwa na klabu ya Al-Ettifaq huku klabu hiyo ya Saudi Pro League ikitafutakuiziba nafasi ya kiungo wa kati wa Uingereza Jordan Henderson, 33, kufuatia kuhamia kwake Ajax. (Liverpool Echo)

TH

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta ametuliza matumaini ya mashabiki ya uwezekano wa shughuli nyingi za usajili katika dirisha la Januari, huku The Gunners wakisita kulipa bei inayotakiwa kumnunua mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 27. (Mirror)

Newcastle na Borussia Dortmund watajaribu kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ufaransa Desire Doue mwenye umri wa miaka 18 kutoka Rennes kabla ya dirisha la usajili la Januari kufungwa. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Aston Villa wamewasilisha ofa mpya kwa Middlesbrough kwa kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Rogers, 21. (Fabrizio Romano)

Manchester City wako katika nafasi nzuri iwapo watalenga watamnunua winga wa Brazil Savio kwa kuwa yuko kwa mkopo katika klabu ya Girona ya Uhispania kutoka klabu ya Troyes ya Ufaransa, vilabu viwili ambavyo viko katika Kundi la City Football Group.

Post a Comment

Previous Post Next Post