WALALAMIKA KULISHWA SUPU YA MBWA



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Moris Makoi amesema kuna tabia ya baadhi ya watu kuchinja mbwa na kuuza nyama kwenye mabucha huku wengine wakichemsha supu ya mbwa na ndizi na kuwauzia watu wakidai ni supu ya nyama ya ng’ombe. 

Akizungumza kuhusu tatizo hilo Makoi amewataka watumishi wa Idara ya Afya kuimarisha usimamizi wa utoaji wa vibali vya kusafirisha wanyama, kukagua na kusimamia mabucha kwani kuna wafanyabiashara wanaweka nyama ya ng’ombe yenye mihuri mbele ya mabucha huku ndani wakiweka vibudu. 

Idara ya Afya katika halmashauri ya Wilaya ya Moshi imesema operesheni ya kukagua mabucha ya nyama ili kubaini wafanyabiashara wanaouza nyama ya mbwa tayari imeanza huku Mganga Mkuu wa Halmashauri, Alex Kazula akibainisha kuwa wameanza kufanya ukaguzi kwenye maeneo yanayodaiwa  kuwa na tatizo hilo ikiwemo Kata ya Kibosho Kati, Okaoni na Kirima.

Post a Comment

Previous Post Next Post