RC MONGELA ATAKA KUKAMATWA KWA MKANDARASI ARUSHA


RC MONGELA AWASWEKA NDANI WAKANDARASI WA MRADI WA UMEME WA KV 400 KISA TANESCO

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ameagiza kukamatwa  na kuswekwa ndani wakandarasi wa wawili wa mradi wa kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovolti 400 unaounganisha nchi ya Tanzania na Kenya baada ya Wakandarasi hao kushindwa kukamilisha mradi kwa wakati huku pia wakigoma kuwalipa mishahara ya miezi miezi kadhaa wafanyakazi wanaohudumu kwenye mradi huo.

Aidha RC Mongela alionesha kuchukizwa na namna shirika la umeme nchini TANESCO lilivyoshindwa kuwasaidia Wafanyakazi  hao kupata stahiki zao, huku wakivunjiwa mikataba na kulazimishwa kusaini na kampuni mpya ya kuwasimamiia.

Mongela alifikia hatua hiyo ya kuwaagiza polisi kuwakamata mabosi wa kampuni hiyo baada ya kushindwa kuridhishwa na maelezo yao, huku wakimuonyesha dharau wakati alipofanya ziara ya kikazi kwenye mradi huo.

Wakandarasi waliokamatwa ni wale wanaojenga Kituo kikuu cha kupozea umeme eneo la kisongo jijini Arusha

Awali wafanyakazi hao wakieleza kero zao kwa mkuu wa mkoa, wamesema Wamekuwa wakinyimwa stahiki zao na kuambulia mateso.

Mradi huo wa kusafirisha umeme wa KV400 Kutoka Singida Hadi Namanga unafahamika kama (Kenya-Tanzania Power Interconnector Project ), (KTPIP ) ulikuwa ukamilike tangu mwaka 2020 na unaelezwa ungeisaidia Tanzania kuwa na umeme wa kutosha na kuuza nje ya nchi.




Post a Comment

Previous Post Next Post