MUSK KUWEKEZA TANZANIA



Tovuti ya Starlink inayomilikiwa na mfanyabiashara bilionea ambaye pia ni mmiliki wa Mtandao wa Twitter, Elon Musk imetangaza mpango wa kuleta huduma ya intaneti kwa njia ya satelaiti (starlink) nchini Tanzania kati ya Januari na Machi 2023 endapo itaruhusiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA), Dk Jabiri Bakari amethibitisha kuwa kampuni hiyo ya Starlink ilituma maombi ya kutoa huduma ya intaneti nchini kupitia tovuti ya TCRA.

Bilionea Elon Musk ambaye ni raia wa Marekani anamiliki vitu vingi hasa vya kiteknolojia yakiwemo magari ya kutumia umeme na ndiye mmiliki wa Program ya Starlink ambayo ni mkusanyiko wa satelaiti nyingi angani ambao humpa mtu huduma za chaneli zinazoweza kumpatia internet yenye spidi ya hali ya juu zaidi duniani.

Inaelezwa kwamba, kwa sekunde moja, program hiyo inaweza kumsaidia mtu kupakua hadi GB 100 maana yake ni kwamba ili kupata huduma ya intaneti huhitaji kuwa na minara ya simu kama ilivyo sasa, unakuwa na dishi tu kisha unalipia, unapewa chaneli na unapata huduma ya intaneti.

Post a Comment

Previous Post Next Post