ATLAS MARATHON KUFANYIKA OKTOBA 14



Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Atlas Day (Atlas Half Marathon 2022, Graduation na Exhibition) Annah Lupemba akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mark Group na Shule za Atlas Sylivanus Rugambwa na wadau wengine wakwa katika picha ya pamoja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Atlas Day (Atlas Half Marathon 2022, Graduation na Exhibition) Annah Lupemba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mark Group na Shule za Atlas Sylivanus Rugambwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

UONGOZI wa Shule za Atlas umesema mbio za Atlas Schools Marathon kwa mwaka huu zitasaidia kuboresha miundombinu ya matibabu kwa mama na mtoto katika hospital inayohudumia wakazi wa Madale na maeneo jirani ya Flamingo Hospital jijini Dar es Salaam. 

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 11, 2022 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Atlas Day (Atlas Half Marathon 2022, Graduation na Exhibition) Annah Lupemba akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Siku ya Atlas (Atlas Day) na Atlas Schools Half Marathon itakayofanyika Oktoba 14 mwaka huu.

"Katika kufanikisha jambo hili muhimu tunapenda kuwatangazia wadau na umma wa watanzania kwamba sasa rasmi Atlas Day, Graduation, Maonyesho ya vitu mbalimbali, michezo ya watoto na burudani kemkem zitakazochagizwa na Atlas Half Marathon 2022 itafanyika katika viwanja vya Atlas Schools Madale ambapo tutaanza kuanzia saa 11:00 Alfajiri kwa mbio yaani Atlas Half Marathon na naadae kufuatiwa na na Mahafali yatakayoanza kuanzia saa 4:00 Asubuhi na kuendelea pamoja na uwepo wa matukio mbali mbali," amesema Lupemba na kuongeza,

"Katika Siku hiyo ya Atlas Day tutaanza na Atlas Half Marathon ambapo tutakua na mbio za 21km, 10km na 5km) ambazo mbio hizi zitaanzia hapa hapa katika viwanja vya shule za Atlas Madale na kuhitimishwa hapa hapa (Yaani starting na Finishing Point ni hapa hapa shuleni),".

Kwamba kwa mwaka huu kauli mbiu itakua ni "kimbia kizalendo boresha Afya", Vile vile kwa kuwa mwaka huu  tarehe ya kufanyika kwa mbio hiyo imeangukia siku ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere ambayo ni Oktoba 14, 2022 wameamua matukio hayo yaende sambamba na kusherehekea kumbukizi ya Baba wa Taifa ambapo kama angelikua hai mpaka leo, basi angekua anatimiza miaka 100.

"Hivyo basi kwa kuenzi kazi nzuri alizozifanya katika taifa kwa mwaka huu Marathon yetu ina mambo mengi ambayo yataendana na yale mazuri aliyoyatekeleza kipindi cha  uhai wake.

Lupemba amewakaribisha watakaopenda kushiriki mbio hizi kwa 5km, 10km na 21km kwmaba watapaswa kuchangia ada kidogo ya ushiriki ambayo ni shilingi 30,000 kwa mtu mmoja, na kwa kikundi cha watu wasiopungua 15 watapata punguzo la asilimia 10, hivyo watachangia shilingi 27,000 tu.

Kwamba baada ya kusajili, mshiriki atapata Fulana ya kukimbilia, Namba ya kukimbilia (bib number), na pia njiani atapata huduma zoote muhimu za kukimbia kama vile Maji, Matunda, huduma ya kwanza, wrist band, na atakapomaliza mbio atapatiwa medal nzuri na viburudisho kama vile soup yenye viwango na nyama choma.

Amewahimiza washiriki wakafanya usajili na kufika kuchukua vifaa vyao mapema kwani mpaka sasa wamekwisha sajili washiriki zaidi ya asilimia 80 ambapo lengo lao ni kuwa na washiriki zaidi ya 2000.


Amesema baada ya shughuli ya Marathon kukamilika washiriki wote watapata muda wa kushiriki zoezi la upandaji wa miti ambapo kila mshiriki ataandaliwa mti na eneo maalumu la kuupanda mti wake na kuweka alama ya ushiriki wake katika marathon ya mwaka huu wa 2022. 

Vile vile amesema kutakua na burudani kem kem kama vile, Soup, nyama choma, maonyesho ya bidhaa mbalimbali, Muziki Mzuri wa Djs, huduma ya chakula na vinywaji na burudani kemkem kuendelea kwa siku nzima.

Pia amebainisha watakuwa na sherehe za Mahafali ya 17 ya shule za Atlas ambapo wanafuzi zaidi ya 700 watakua wakitunukiwa tunzo baada ya kuhitimu elimu hao ikiwa ni pamoja na wahitimu wa Nursery, Darasa la Saba na Kidato cha nne. Wahitimu wetu kutoka katika shule zote tatu ya ni Atla Primary Ubungo, Atlas Primary Madale na Atlas Secondary Madale watasherehekea mahafali pamoja na wazazi wao kwa aina tofauti kwani tunatarajia ushiriki wao katika marathon utachagizwa na tunzo mbalimbali ikiwemo medal ambapo mwanafunzi anaweza kutunukiwa cheti na medal ya kukimbia marathon nabikawa kumbukumbu nzuri kwake na Mzazi wake. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mark Group na Shule za Atlas Sylivanus Rugambwa amesema kwa kujali ushiriki wa wakimbiaji wa aina mbalimbali, kamati ya maandalizi imeandaa zawadi maalumu kwa msimu huu kwa watoto na Wazee wa umli kuanzia miaka 60 nankuendelea. 



"Mwaka huu tutakua na zawadi kwa washindi watano wa kila mbio na jinsia kwa watoto na wazee wa umri miaka kuanzia 60 na kuendele. Kamati ilipendekeza haya ili kuenzi kumbukizi ya miaka 100 ya Mwl. Nyerere ambapo tunaamini Mwalimu aliwapenda watoto na pia kuwapa Pongezi wale wazee ambao kwa namna moja au nyingine walishuhudia kazi za Nyerere au walishiriki katika kazi na baba wa taifa kipindi hicho," amesema Rugambwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post